MWANA HABARI WA KIKE APIGWA BUSU KWA KULAZIMISHWA URUSSI LJ P

Mwanahabari mmoja wa kike amepigwa busu kwa lazima na kunyanyaswa akifanya ripoti kuhusu Kombe la Dunia.
Mtangazaji huyo raia wa Colombia Julieth Gonzalez Theran alikuwa akitangazia moja kwa moja shirika la Habari la DW Espanol .
Tukio hilo limetokea mjini Moscow wakati mwanaume mmoja alipojitokeza na kumshika maziwa kabla ya kumpiga busu.
Ingawa Julieth aliendelea na kazi yake, alililizungumzia tukio hilo baadaye.
"Sikustahili kutendewa vile," Gonzalez Theran alisema. "Tuko na thamani na weledi pia."

Amemueleza mwajiri wake, Deutsche Welle, alikuwa eneo la tukio kwa muda wa saa mbili akijiandaa.
"Tulipoanza kupeperusha matangazo, shabiki mmoja alichukua fursa hiyo," aliongeza. "Lakini baadaye, nilipoangalia kuona iwapo alikuwa eneo lile, sikumuona."
Kisa hicho kilitokea juma lililopita mjini Saransk kabla ya mechi kati ya Russia na Saudi Arabia.
DW iliweka kanda ya video ya tukio hilo kwenye mtandano na kushutumu tukio hilo kuwa "uvamizi" na "unyanyasaji".
Hata hivyo wengine wameita tukio hilo kuwa la kawaida.
"Kulingana na mimi, sio kawaida," Gonzalez Theran alifafanua. "Kuna watazamaji wa kukushabikia kwa ustaarabu, hili lilivuka mpaka."
"Si mzaha," Mtangazaji wa DW Cristina Cubas aliandika kwenye twitter. "Si busu. Ni uvamizi."
Unyanyasaji wa watangazaji wa kike sio jambo geni kwneye michezo.
Mwaka uliopita mchezaji wa tenisi Maxime Hamou alipigwa maruuku kutoka kombe la French Open baada ya kumbusu mtangazaji wa kike kwa lazima kwenye mahojiano ya moja kwa moja.
"Iwapo singekuwa hewani, ningempiga ngumi ," alisema mtangazaji huyo, Maly Thomas, baada ya tukio.
LihatTutupKomentar