SAMATTA AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA NYONI

Nyota wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya soka ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubeligji, Mbwana Samatta amefunguka kuhusu suala la umri kwa wachezaji na kusema kumbe ni namba tu.

Samatta ametumia mtandao wa Twitter kueleza hilo wakati akionesha kuridhishwa na kiwango cha mchezaji mkongwe wa Tanzania Erasto Nyoni, ambaye Jumapili alifunga bao pekee kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga.
Samatta aliandika ''Erasto Nyoni (umri ni namba tu kumbe)'',. Hatua hiyo imechukuliwa kama sehemu ya nyota huyo kutambua kiwango cha kiraka huyo wa Simba ambaye amecheza kwa misimu mingi katika kiwango cha juu.

Erasto Nyoni aliifungia Simba bao lililowapa alama tatu kwenye mchezo wa ligi kuu Jumapili iliyopita dhidi ya Yanga. Bao hilo alifunga dakika ya 37 kipindi cha kwanza.

Nyoni ameshawahi kuzichezea klabu tofauti tofauti hapa nchini na nje ikiwemno A.F.C Arusha, Azam FC na sasa Simba huku nje akiichezea Vital'O ya Burundi.

LihatTutupKomentar