SABABU ZA LIVERPOOL KUFUNGWA NA REAL MADRID HIZI

Na:MOSES FRANCIS
Katika jiji la Kiev lililopo nchini Ukrane timu ya Liverpool ilikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa wapinzani wao Real Madrid. Kuna sababu nyingi za kitaalamu ambazo zilipelekea Liverpool kupoteza pambano hilo, lakini mimi nitasema sababu chache. Kwanza kabisa Liverpool haina kikosi kipana, nasema hivyo kwasababu kuumia kwa Mohamed Salah dakika 30 na kutolewa nje kuridhihirisha pengo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Liverpool. Awali kabla ya kutolewa kwa Mohamed Salah timu ilionekana kucheza kwa kujiamini huku ikishambulia kwa kasi zaidiKupitia kwa Sadio Mane, Roberto Firmino, pamoja na Mohamed Salah. Lakini badae Tunamwona Mohamed Salah anatoka anaingia Adam Lallana ambaye anashindwa kuleta madhara makubwa katika safu ya ulinzi ya Real Madrid. Hiyo ndio tafsiri ya kuwa na kikosi finyu kwasababu Adam Lallana alipaswa awe na mchango angalau nusu kama wa Mohamed Salah lakini hana uwezo huo, kwa maana hiyo pengo la Mohamed Salah lilionekana kuonekana japokuwa Adam Lalana aliingia kuchukua nafasi yake. Sababu ya pili safu ya kiungo ya Liverpool ikiongozwa na Jordan Henderson haikuonekana kucheza vyema zaidi na hii ilikuja baada ya viungowa Real Madrid kina Casemiro, pamoja Luca Modric, ambao walionekana kucheza kwa kujiamini zaidi pasipo kukumbana na upinzani kutoka kwa viungo wa Liverpool ambao walionekana kurudi nyuma zaidi na hii ilikuja baada ya Mohamed Salah kuwa ametoka, na hivyo iliwabidi Liverpool waanze kucheza mipira mirefu kwenda pembeni kwa Sadio Mane, pamoja na Adam Lallana kwa maana hiyo hapakuwepo na nafasi ya kutengeneza nafasi kupitia katikati ( mildfield). Ukijaribu Kutazama hata goli ambalo Liverpool kupitia kwa Sadio Mane lilitokana mpira mrefu ambao unapigwa kuelekea katika lango la Real Madrid lakini katikaharakati za kuokoa mpira huo Sadio Mane anauwahi mpira na anafunga. Magoli ya namna hii Liverpool wamekuwa hawayafungi sana msimu huu. Magoli mengi wamekuwa wakiyatengeneza kuanzia katikati kwenye mildfield. Sababu ya tatu ya ni makosa ya golikipa Karius ambaye kwa namna moja au nyingine aliigharimu timu. Goli la kwanza ambalo Benzema anafunga linatokana na uzembe pamoja na kutokuwa makini katika kuanzisha mpira kwenda kwa mabeki wake, na badae tunamwona Benzema anatega mguu wake ambao unakutana na mpira na anafunga kirahisi tu. Goli la tatu ambalo Real Madrid wanalipata kupitia kwa Gareth Bale pia ni mapungufu ya golikipa Karius kwasababu Gareth Bale ni sawa alipiga shuti kali lakini kwa umbali aliokuwa Bale pamoja na Karius kulikuwepo na uwezekano wa kuucheza mpira ule kwa kuupangua kwa nguvu au kuudaka, nasema hivyo kwa sababu ni mpira ambao ulimlenga golikipa karius. Mipira ya namna ile ni vigumu kumfunga golikipa kama Manuel Neuer, David Degea, au Gigg Buffon. Mwisho Liverpool walicheza vyema sana katika safu yao ya ulinzi ikiongozwa na Lovren, Virgil, Anord Alexander pamoja na Andrew Robertson. Ni bao moja tu ambalo limetokana na mapungufu ya safu ya ulinzi ya Liverpool ni bao la tik tak la Bal
LihatTutupKomentar