AZAM FC LAZIMA YANGA TUWALIPE DENI LAO

WAKATI kikosi cha Azam FC kikiwa kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo ujao dhidi ya Yanga, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa amepanga kuonyesha mchezo mzuri na kulipa kisasi cha kufungwa ule wa kwanza.
Mchezo huo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unatarajia kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatatu hii saa 2.00 usiku.
Cheche ameonyesha kuiheshimu Yanga akiamini kuwa mchezo utakuwa mgumu na mzuri huku akiwaomba mashabiki wa soka wajitokeze kushuhudia burudani.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Azam FC iliteleza na kufungwa mabao 2-1, bao la Azam FC likifungwa na mshambuliaji Shaaban Idd huku yale ya Yanga yakitupiwa na Gadiel Michael na Obrey Chirwa.
“Mechi ya kwanza imeshapita, japokuwa inamajeraha kwetu lakini tuna mechi ya marudiano hii nafikiri tunaenda kulipiza lile deni ambalo tuliokuwa nalo, kwa sababu walituachia deni hatuna budi kulilipa kuhakikisha tunalipa mabao waliyotufunga ikiwezekana kuongeza zaidi ya yale,” alisema.
Asifia umoja
Azam FC imetoka kushinda mechi mbili mfululizo, ikiichapa Majimaji (2-0) na Tanzania Prisons (4-1), akizungumzia siri ya mafanikio hayo, alisema imetokana na ushirikiano na umoja ulioko kwenye timu hiyo.
“Ni umoja tu katika kazi kwenye kazi mkiwa wamoja mnashirikiana, mnafanya kazi pamoja, mnapendana nafikiri matokeo yanapatikana, ushirikiano na umoja ndio unatusaidia katika haya yote,” alisema.
Hadi kuelekea mchezo huo wa mwisho wa ligi, timu hizo ziko kwenye vita kali ya kuwania nafasi ya pili, Azam FC ikiwa inaishikilia kwa pointi zake 55 
LihatTutupKomentar