ENEMY INAI ANA KAZI YA KUFANYA ARSENAL


Mchana wa leo mabosi wa klabu ya arsenal wamemtangaza kocha ENERY INAI kuwa kocha mkuu wa arsenal. Ni maamuzi sahihi ambayo arsenal wameyafanya. Mabosi wa klabu ya arsenal wameenda kwa kocha mzoefu,Inai ni kocha ambaye ametamba katika michuano ya ulaya akiwa na klabu ya sevilla.Inai ametwaa kombe la europa mara mbili, Inai amefika hatua ya nusu fainali klabu bingwa akiwa na psg, Inai ametwaa ubingwa wa ligi kuu ufaransa msimu huu. Arsenal walikuwa wanamhitaji kocha wa namna hii na si kina Mikel Arteta kama jinsi walivyokuwa wakiaminishwa.Kina Arteta pamoja na washikaji zake kina Patrick Vieira bado ni makocha wachanga katika ukocha. Kwa mfano Arteta hana hata miaka 5 tangu asitaafu soka na hajawahi kufundisha hata timu daraja la pili halafu leo hii apewe arsenal?  Jibu ni hapana.kwa sasa ENERY Inai ana kazi ya kufanya pale arsenal. Kwanza ana kibarua cha kuirudiasha arsenal katika michuano ya ulaya msimu ujao, pia anakazi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi  kuu uingereza ubingwa ambao arsenal wanausikia tu siku za hivi karibuni.

LihatTutupKomentar