YANGA YASHINDWA KUTAMBA MBEYA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania timu ya Yanga imelazimishwa sare ya bao moja na Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa Sokoine.
Wenyeji City walitoka nyuma na kusawazisha bao dakika ya 90 kupitia kwa Idd Suleiman ' kwa kichwa baada ya kupokea pasi ya Kenny Kunambi.
Jana watani wao wa jadi Simba walilazimishwa sare kama hiyo na Lipuli FC katika mchezo uliofanyika uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Yanga ilipata bao lake dakika ya 58 kupitia kwa Raphael Daud akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Juma Abdul.
Mchezo huo iliingia doa kutokana na fujo kutoka kwa mashabiki wa City baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi Shomari Lawi alipomtoa Ramadhan Malima dakika ya 65.
Baada ya kadi hiyo mpira ulisimama kwa dakika sita kufuatia mashabiki kurusha mawe uwanjani ambayo baadhi yalimpiga mlinda mlango wa Yanga, Youthe Rostand.
Yanga imeendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 48 ikizidiwa 11 watani wao Simba.

LihatTutupKomentar