YANGA KUWAFATA MBEYA CITY LEO

Na Emmanuel mkome (Mr Arsenal)

Mabingwa wa soka tanzania bara mara tatu mfululizo timu ya Yanga baada ya kuwasili jana (Ijumaa) wakitokea nchini Ethiopia kwenye mchezo wa kombe la shirikisho la CAF dhidi ya Walayta Dicha,leo wanasafiri kuelekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu  dhidi  ya mbeya ambao ni wenyeji wa mchezo huo,mchezo ambao umepangwa kupigwa jumapili (kesho) kwenye uwanja wa Sokoine.

Kaimu kocha mkuu Noel Mwandilla amesema kuwa hali ya kikosi chake si mbaya licha ya safari na mchezo mgumu wa kombe la shirikisho na wako tayari kwa ajili ya upambanakuhakikisha timu inapata alama tatu ambazo ni muhimu kwenye mchezo huo wa ugenini.

Kwa upande wa kikosi cha Yanga,kiungo papy kambamba hatakuwa sehemu ya mchezo huo wa jumapili (kesho) baada ya kupata majeruhi ya mguu wa kulia aliyopata kwenye mchezo wa  kombe la shirikisho  dhidi ya Welayta Dicha,wakati Ibrahim Ajib akitarajia kushuka dimbani  baada ya kupona.

Ifahamike kuwa Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kufanikiwa kuitoa Welayta Dicha kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1.

LihatTutupKomentar