YANGA KUJA KIVINGINE MSIMU UJAO

Licha ya Kufuzu kucheza hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika  Klabu ya Yanga SC Imekuwa ikisuasua katika baadhi ya Mechi zake Sababu za kiuchumi ndani ya Klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa Klabu hiyo ya Jangwani Charles Boniphace MKWASA Amesema kuwa kikosi Chao kitakuwa na Mabadiliko hivyo Wanatajia kuwa Vizuri Msimu Ujao.
Tatizo la kiuchumi ndani ya Yanga SC lilikua Mara baada tu ya Akiyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Maheeb Manji kujiengua katika Nafasi hiyo ya Uwenyekiti.
Akiongea Mkwasa Amesema kuwa Yanga ni Klabu kubwa Tanzania japokuwa msimu huu imefanya vibaya lakini Msimu Ujao itarejea ikiwa na Nguvu.

"Tumeandaa kitu kizuri kwa msimu Ujao,tutarejea katika kiwango chetu na kuwarudisha Mashabiki wetu Ambao Msimu huu wamekata tamaa na Klabu"

Alisema Mkwasa Anaefahamika kwa jina la "Master".
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kufunga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwatoa Wahabeshi Welayta Dicha Kutoka Ethiopia kwa Ushindi wa jumla ya Magoli Mawili kwa moja, Na katika ligi Kuu ipo Nafasi ya pili Pointi 11 Nyuma ya Vinara Simba SC.

LihatTutupKomentar