SANGA SIMBA HAITUTISHI

Na EMMANUEL MKOME: (Mr Arsenal)
Timu ya soka ya ya mkoani iringa  Lipuli fc imeendelea na mazoezi kwaajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya simba  sc utakochezwa tarehe 21 mwezi huu (jumamosi hii) katika uwanja wa samora
msemaji wa timu ya lipuli fc clement sanga amesema kuwa timu inaendelea vyema na mazoezi kwaajili kuwaweka wachezaji katika hali ya kupambana zaidi na mchezo huo
"mchezo huo ni mgumu kwakuwa unatukutanisha na timu ambayo ipo katika mbio za kuelekea kutwaa ubingwa wa vpl lakini hawatutishi hata kidogo tutapambana kadri ya uwezo  wetu " alisema sanga
ikumbukwe kwamba lipuli inacheza huo ikitoka kuwafunga singida united ya mkoani singida goli 1-0 katika mchezo wa ligi kuu bara jumapili ya wiki iliyopita mchezo uliyo chezwa mkoani  iringa kwenye uwanja wa samora
kwenye msimamo wa ligi kuu tanzania bara lipuli fc iko katika nafasi nane(8)  uku ikiwa imecheza michezo 25 Ikiwa imekusanya alama 31,huku simba akiwa kileleni mwa ligi akiwa na alama 58 akiwa amecheza michezo 24.
LihatTutupKomentar