MASHUJAA WALIOWAKILISHA VEMA MIKOA YAO



na Gharib MZINGA
Nchi ya tanzania, Dar es salaam ni miongoni mwa mikoa yenye Eneo dogo la Aedhi, Lakini ndio mkoa unaoongoza kwa idadi kubwa ya watu. Mambo mengi ya kimaendeleo huanzia hapa. Hapa kuna uwanja mkubwa wa Soka wa nchi, Hapa kuna makao makuu ya soka ya taifa, Hapa kuna Vilabu nguli vikongwe nchini, Hapa kila mchezaji anatamani siku moja aishi katika jiji hilo.

Hiyo ndio Dar es salaam BWANA.

Licha ya hayo yote Dar es salaam ndio mkoa unaoongoza kwa kutoa timu nyingi zilizowahi kushiriki ligi kuu tanzania bara.  Halina mjadala hilo. Watanzania wamegawanyika katika timu mbili Tu. Nazo ni Simba na Yanga.

Mbali na Dar es salaam kuwa na vitu vyote hivyo, Bado kuna mashujaa wengine ambao wapo nje ya Dar es salaam Na waliwahi kuiwakilisha vema mikoa yao Mithiri ya Mtolewa alivyoiwakilisha Ardhi ya Giningi chini ya Utawala wa Bi kirembwe wa kivuli kinaishi.

Umewahi kusikia Timu ya Pamba Fc ? Kutoka mwanza? Hawa walifaamika zaidi kwa jina la Tupwisa Lindanda. Timu hii iliundwa miaka ya 1960s chini ya Bodi ya Pamba Mwanza. Mwaka 1970 ilipanda daraja la kwanza (ligi kuu sasa) baadhi ya wachezaji wake ni George masatu, Khalfan Ngassa, David mwakalebela, Fumo Felician na wengine wengi.  Licha ya uwepo wa Mbao na Toto africa, Bado Pamba imeacha kumbukumbu kubwa. Iliitwa Brazil ya Tanzania.

Karibu dimba la Ilulu, Timu nyingi nguli zilijaribu kutafuta alama katika uwanja  huo lakini zilichemka. Kariakoo fc alikua mgumu katika dimba la nyumbani, Kariakoo ndio Kiwakilishi cha pekee mkoani Lindi, Pia ni mshindi wa kombe la Headex mwaka 1999-2000 baada ya kuilaza Mlandege Goli 3-1. Wana lindi wanaikumbuka sana timu hii.

Ushirika moshi kwa sasa haipo ligi kuu, Hawa walikua na sifa ya kutandaza kandanda safi sana, Licha ya kutokua na mafanikio makubwa, ndio timu pekee iliyoacha kumbukumbu kubwa pale Moshi na kilimanjaro kwa ujumla.

Tukuyu stars banyambala, Kikosi cha Asanga aswile, Mbwana makata, Betwel africa, Chachala Muya, Daniel Chundu. Ni miongoni mwa mashujaa waliowahi kutokea Mkoani mbeya, Tukuyu stars ilipanda ligi daraja la kwanza mwaka 1986 wakabeba na ubingwa msimu wa 1988 ikashuka daraja. Hawa waliiwakilisha vema Mbeya. Ukizungumzia mbeya kisoka Utaizungumzia Tukuyu stars.

Kigoma, Miongoni mwa mikoa yenye vipaji vingi sana tanza nia. RTC kigoma na RELI ndio vilabu vilivyoacha kumbukumbu kubwa katika soka mkoani Humo. Kwa sasa Havipo katika ramani.

Ukizungumzia Mtwara kwa sasa utaitaja Ndanda sc, Lakini ifahamike kwamba Wazee wa Mtwara ukiwauliza Timu gani ambayo ni bora kwa muda wote Watakujibu NYOTA mtwara. Hawa ndio walioiwakilisha vema mtwara. Walidumu ligi kuu na walitoa wachezaji wengi kujiunga na timu mbali mbali.

Tanga ni miongoni mwa mikoa yenye ardhiya soka, Licha ya kutoa timu nyingi ligi kuu Coastal union ndio Muwakilishi mkubwa wa mkoa huo mwaka 1988 ilichukua ubingwa wa ligi daraja la kwanza (sasa ligi kuu). ukitaja tanga unaitaja coastal.

CDA na Kurugenzi, ndio miamba iliyowakilisha vema Dodoma. Licha ya kutopata mafanikio makubwa kitaifa.

Tabora, Walikua na Mirambo fc. Mashujaa wa unyanyembe. Hawa Waliiwakilisha vema Tabora pia haikufanya makubwa kitaifa.

Morogoro, Mtibwa Sugar ni timu inayoiwakilisha vema Mkoa wa Morogoro lakini Sio wa kwanza kufanya ivyo. Mseto na Reli Morogoro zilipata mafanikio pia katika kandanda la nchi Hii. Mtibwa imekuja kuendeleza mafanikio.

LihatTutupKomentar