FULL TIMEMchezo umemalizika.
Dk ya 91: Rostand anapewa kadi ya njano kw akupoteza muda.
Dk ya 90: Zinaongezwa dakika tatu za nyongeza.
Dk ya 89: Mashabiki wa Dicha hawaamini macho yao. Matokeo yakibaki hivi timu yao inakuwa imetolewa.
Dk ya 87: Dicha wanacheza faulo, inapigwa kuelekea kwao.
Dk ya 85: Kipa wa Yanga, Rostand kaumia, mchezo umesimama kwa muda.
Dk ya 80: Wachezaji wa Yanga wameanza kupunguza kasi ya wapinzani kwa kumiliki mpira muda mwingi.
Dk ya 76: Kipa wa Yanga anawahi mpira uliopigwa langoni kwake.
Dk ya 75: Chirwa anabaki na wlainzi wanne anashindwa kuwapita.
Dk ya 72: Mhilu anachezwa faulo, inapigwa kuelekea kwa Dicha, mchezo umesimama kwa muda.
Dk ya 70: Mchezo sasa unachezwa kibabe, muda mwingi nguvu zinatumika.Dk ya 52: Mchezo unaanza kuwa mkali.
Dk ya 50: Yanga wanapiga pasi kadhaa.
Dk ya 48: Yanga wanafika langoni mwa Dicha.
Dk ya 46: Kasi ya Dicha imepungua.
Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia uwanjani. time
Dk ya 38: Tshishimbi anakosa nafasi ya wazi shuti lake linapaa juu ya lango.Dk ya 36: Kasi ya wageni imepungua.
Dk ya 31: Bado matokeo ni 0-0.
Dk ya 29: Dicha wanakosa nafasi ya wazi wakiwa wao na lango, mpira unatoka
Dk ya 26: Yanga wanafanya shambulizi kali inakuwa kona.
Dk ya 26: Rostand anadaka shuti kali.
Dk ya 24: Shambulizi kali langoni mwa Yanga lakini kipa Rostand anafanya kazi nzuri.
Dk ya 20: Yanga wanatulia na kupiga pasi kadhaa.
Dk ya 18: Shambulizi kali langoni mwa Yanga, wenyeji wanakosa nafasi ya wazi.
Dk ya 15 Mchezo ni mkali na wenyeji wanaongeza kasi
Dk ya 8: Yanga wanajipanga na kujibu mashambulizi.
Dk ya 3: Dicha wanashambulia kwa kasi kubwa.
Yanga wanaruhusu bao baada ya mpira wa kona kuwapita walinzi kabla ya kujaa wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 1. Dicha wanapata kona.
Mchezo unaanza kwa kasi.