Lipuli FC YAWABANIA SIMBA

Vinara wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba imeambulia pointi moja mkoani Iringa baada ya kulazimishwa sare ya bao moja na Lipuli FC katika uwanja wa Samora.
Simba ilitoka nyuma na kusawazisha bao la kipindi cha kwanza lililofungwa na mshambuliji Adam Salamba ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kwa mwezi Machi dakika ya 31.
Laudit Mavugo ndiye aliyefunga bao hilo dakika ya 66 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na mlinzi wa Shomari Kapombe.
Simba imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 59 alama 12 mbele ya Yanga iliyo nafasi ya pili.
Katika mchezo huo timu zote zilionyesha ushindani mkubwa huku walinda milango wakiwa na kazi ya kuokoa mashuti yaliyokuwa yameelekezwa langoni.
Simba inarejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya watani wao wa Yanga wikiendi ijayo Aprili 29.

LihatTutupKomentar