KOCHA WA YANGA KUHUSU MECHI YA WATANI WAJADI

Yanga imemleta kocha mpya ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na George Lwandamina aliyetimka ghafla na kuelekea Zambia kujiunga na ZESCO United.
Kocha mpya wa Yanga Zahera Mwinyi yupo nchini tangu Jumanne Aprili 24 na tayari yupo Morogoro ambako Yanga imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba Aprili 29, 2018.

Watu wanachotamani kujua ni kwamba, kocha huyo atakuwa kwenye benchi la ufundi la Yanga siku ya Dar derby? Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amefafanua kuhusu jambo hilo.

“Taratibu za kazi zinajulikana nchini hii, lazima taratibu za nchi zifuatwe kwa sababu yeye ni mgeni anapofika lazima apatiwe kibali cha kufanya kazi kwa hiyo saizi ni mapema kusema chochote”-Charles Boniface Mkwasa, Katibu Yanga.
“Anaweza kuangaliatu timu ikoje na inakwendaje.

LihatTutupKomentar