CHIRWA KUIKOSA SIMBA VS YANGA

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Obrey Chirwa, jana amefikisha idadi ya kuwa na kadi tatu za njano katika ligi.
Chirwa ambaye ni raia wa Zambia, amekosa sifa ya kuichezea Yanga katika mchezo ujao dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Aprili 29 2018.
Mshambuliaji huyo atakuwa anatumikia adhabu hiyo ya kuwa na kadi hizo, ambapo kwa mujibu wa kanuni za soka mchezaji hukosa mechi moja inayofuata kwenye ligi inapotokea amefikisha kadi tatu za njano.
Chirwa alipata kadi hiyo katika mchezo wa uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Yanga ilipocheza dhidi ya Mbeya City.


LihatTutupKomentar