BODI YA LIGI YAWAFANYIA UMAFIA YANGA

Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeipangia Yanga kucheza na Mbeya City FC katika mchezo wa Ligi Kuu, ratiba ambayo itakuwa inawabana kutokana na kukosa muda wa kupumzika baada ya kurejea kutoka Ethiopia.
Yanga ambayo inacheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kesho dhidi ya Wolaita Dicha FC, itapaswa kuunganisha moja kwa moja kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo wa ligi utakaopigwa Aprili 22 2018 Jumatatu ya wiki ijayo.
Mbali na Yanga, mchezo mwingine uliofanyiwa mabadiliko ni ule wa Simba SC dhidi ya Lipuli FC kusogezwa mbele.
Mchezo huo ulipaswa kupigwa Ijumaa ya tarehe Aprili 20 2018 Ijumaa ya wiki na sasa badala yake utapigwa Aprili 21 Jumamosi kutokana na wamiliki wa Uwanja wa Samora kuutumia Uwanja huo kwa shughuli zingine za kijamii.

LihatTutupKomentar