ARSENE WENGER ATANGAZA UAMZI MGUMU

Kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wenger leo Ijumaa ya April 20 2018 ametangaza maamuzi ambayo yamewashitua wengi kutokana na kudumu na club ya Arsenal kwa miaka ming
Leo kocha Arsene Wenger baada ya kuifundisha club hiyo kwa miaka 22 toka alipojiunga nayo mwaka 1996 akitokea Nagoya Grampus ya Japan, ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi ya ukocha wa timu hiyo na kuwa ataondoka katika club hiyo baada ya msimu kumalizika.
Wenger ametangaza kufikia maamuzi hayo baada ya kukaa kwa kina na kujadiliana na viongozi wa Arsenal licha ya kuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Arsenal ili umalizike.
“Baada ya majadiliano ya kina na club, nahisi sasa ni wakati sahihi kwa mimi kuachia ngazi mwisho wa msimu huu”>>>> Wenger

LihatTutupKomentar