Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameomba wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuendeleza umoja ndani ya timu yao ili iweze kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Simba.
Akilimali ameomba hilo kufanyika zikiwa zimesalia siku tatu pekee kukutana kwa watani hao wa jadi, Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Aidha, Akilimali amesema vijana wao wap kambini na wanaandaa dozi maalum ya Simba watakayopewa Jumapili ya wiki hii.
Mechi hiyo yenye hisia kubwa kwa mashabiki na wadau wa soka kwa ujumla nchini, itapigwa Aprili 29 katika Uwanja wa Taifa.