Yanga Watua Salama Shelisheli


KIKOSI cha mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga kimetua salama kwenye mji wa Victoria nchini Shelisheli tayari kwa mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya St. Louis.


Mechi hiyo inayotabiriwa kuwa ya kukata na shoka inatarajiwa kupigwa Jumatano ya Februari 21 huku Yanga wakihitaji japo sare ya aina yoyote ili wasonge mbele kwa faida ya ushindi wao wa bao 1-0 walioupata jijini Dar.
LihatTutupKomentar