20 KUIFUATA GENDARMARIE, BOCCO NDANI


Klabu ya Simba jioni ya leo majira ya Saa 11:00 jioni imeondoka na ndege ya shirika la KQ kuelekea Djibout kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Gendarmerie Nationale mchezo utaofanyika Djibout siku ya Jumatano February 21.

Simba imeondoka nyota 20 akiwepo Mshambuliaji wa klabu hiyo John Bocco ambaye ni majeruhi kwa mjibu wa  bechi la ufundi la klabu hiyo wameamua kwenda na Bocco ili asikose program za mwalimu ila atakuwa chini ya Uangalizi wa madaktari wa klabu hiyo

wachezaji ambao wameondoka  ni Makipa:- Aishi Salum Manula, Emmanuel Mseja  Mabeki:- Shomary Kapombe, Ally Shomary, Hussein Mohamed, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Paul Bukaba Viungo ni :- Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto, Na Shiza Kichuya washumbuliaji ni :- John Bocco, Emmanuel Okwi, Moses Kitandu na Nicholas Gyan

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa kombe la shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup) uliofanyika Dar Es Salaam, Simba walishinda kwa mabao manne kwa bila (4-0)

Iwapo Simba Sc itaitoa Gendarmerie Nationale ya Djbout itacheza raundi ya kwanza na mshindi kati ya Elmasry ya Misri na Green Buffaloes Zambia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza  Elmasry waliifunga Green Buffaloes kwa mabao manne kwa bila (4-0) mchezo uliochezwa Misri.

Pia Simba wakifuzu raundi ya kwanza wataanzia mechi yao ugenini. mechi ya mkondo wa kwanza katika raundi ya kwanza  kuchezwa March 9-11 na zile za marudiano ni March 16-18.
LihatTutupKomentar