SIMBA HII HATARI SANA


Timu ya Simba imezima kelele na vijembe vya mashabiki wa Stand United baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Shiza Kichuya pamoja na Laudit Mavugo kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo Jumapili.
Kikosi hicho ambacho kimefanikiwa kuchomoka na pointi tatu muhimu, kimeleta matumaini kwa mashabiki wao baada ya mchezo uliopita kutoka sare ya mabao 2-2 na Mbao FC.
Timu hiyo imepanda kileleni ikiwa imefikisha pointi 11 ambazo zimefikiwa na Azam FC pamoja na Mtibwa huku watani zao Yanga walikwaa kisiki jana baada kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru jana Jumamosi.
Nahodha wa timu hiyo, Mwanjali alisema wanampongeza kipa wao Aishi Manula kwa kuokoa hatari nyingi, huku akisistiza kuyafanyia kazi upungufu uliyojitokea katika kikosi hicho cha leo.
Hata hivyo aliongeza kuwa awali kikosi hicho kililala jambo ambalo liliwapa nafasi wapinzani wao kufunga bao la kufutia machozi
LihatTutupKomentar