Habari toka jangwani


Yanga imewapumzisha washambuliaji wake wawili, Donald Ngoma na Obrey Chirwa kutokana na kuwa majeruhi.

Washambuliaji hao wawili  wamekuwa wakiandamwa na majeruhi na taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, daktari ameamua kuwapumizisha.

"Kikosi kinaendelea na mazoezi kama kawaida lakini Chirwa na Ngoma ambao wamekuwa na maumivu wamepumzishwa kuwapa nafasi ya kuendelea kupata matibabu huku wakijiangalia. Nafikiri wataanza mazoezi Jumatatu," kilieleza chanzo. chetu

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara hawajaanza vizuri lakini bado wana nafasi ya kubadilika kwa kuwa ligi iko mwanzoni kabisa.

Suala la majeruhi au kadi, nalo limekuwa ni sehemu ambayo inamtatiza Kocha George Lwandamina ambaye msimu uliopita ndiye aliyeiwezesha timu hiyo kubeba ubingwa.
LihatTutupKomentar