BECHI LA UFUNDI LA YANGA LAZUNGUMZA HAYA

BENCHI la ufundi la Yanga chini ya kocha wake mkuu, George Lwandamina, limefunguka kuwa linapata simanzi juu ya washambuliaji wao wakiongozwa na Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu kwa kushindwa kufunga mabao kwenye michezo yao ya ligi kuu licha ya kutengeneza na kupata nafasi nyingi za kufunga mabao.
Yanga kwenye michezo yake mitano ya ligi kuu hadi sasa, yenye dakika 450, imefanikiwa kufunga mabao manne pekee, yaliyofungwa na Ngoma pamoja na Ajibu ambao kila mmoja kafunga mawili.
 Jumatatu, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema licha ya kuwapa mbinu mbalimbali washambuliaji wao lakini kwenye mechi wamekuwa wakishindwa kufanyia kazi kile ambacho wanawaambia.
“Bado kuna tatizo kwenye safu yetu ya ushambuliaji kwa sababu haitupi kile ambacho tunakitaka kwenye michezo yetu kutokana na kushindwa kufunga mabao mengi kama ambavyo tunawafundisha na kuwapa mbinu tukiwa mazoezini.
“Nadhani hilo linasababishwa na presha waliyonayo kwa sababu wanacheza wakiwa wanawaza kwamba mashabiki wanataka matokeo na mwisho wake wanajikuta ndiyo wanafanya hivyo, tumeshaliona tatizo na sasa tunaenda kulitafutia tiba zaidi kwa ajili ya kulitatua,” alisema Nsajigwa.
Yanga1
LihatTutupKomentar