kwa lukaku huyu wa moto mjiandae


#KWA_LUKAKU_HUYU_WA_MOTO, MJIANDAE.....
Na francis
Wa mkome sports

MASHABIKI wengi wa klabu ya Manchester United wanaonekana kuwa na furaha kuiona timu yao ikifanikiwa kumnasa mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, huku wachache wakiwa na wasiwasi.

Kwanini wachache wana mashaka? Mbelgiji huyo ana uwezo utakaomfanikisha kuwa mchezaji bora Old Trafford, lakini kuna alama ya kiulizo inayowaandama wengi kuhusu uwezo wa kuzifunga timu kubwa alionao Lukaku.

Msimu uliopita, kati ya mabao 25 aliyofunga EPL, 21 aliyatupia dhidi ya timu 13 za chini.

Lukaku aliisaidia Everton kumaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo, juu yao zikimaliza Chelsea, Tottenham, Manchester City, Liverpool, Arsenal na Manchester United.

Kuanzia nafasi ya nane ambayo ni timu iliyo chini ya Everton, zote zilizobakia Lukaku alizifunga na alikaribia kuwa mfungaji bora kama si balaa la straika wa Spurs, Harry Kane aliyefanya maajabu ndani ya mechi mbili za mwisho za EPL.

Lukaku alikuwa akiongoza msimamo wa wafungaji bora kwa tofauti ya mabao mawili tu (25 kwa 22 ya Kane), lakini Kane aliibuka ghafla na kutupia jumla ya mabao saba ndani ya mechi mbili za mwisho, mabao yaliyomfanikisha kuchukua kiatu cha dhahabu kwa kufikisha mabao 29.

Takwimu ya Lukaku dhidi ya miamba sita ni nzuri mno licha ya kwamba wengi wana wasiwasi.

Katika msimamo wa wafungaji bora, Lukaku aliweza kuifunga miamba mitatu kati ya sita ya EPL, akifunga mawili dhidi ya Man City na mawili dhidi ya Spurs na Arsenal, jumla manne.

Lukaku ndiye mshambuliaji pekee aliyeweza kutikisa nyavu za baadhi ya timu sita za EPL zaidi ya mara mbili, licha ya kwamba katika msimamo wa wafungaji bora, walikuwepo wengine wakali pengine zaidi yake.

Sergio Aguero wa City akitikisa nyavu mara tatu dhidi ya Liverpool, Arsenal na Chelsea, Kane akifunga matatu (mawili dhidi ya Arsenal) na lingine akiwapiga Man United, huku Diego Costa ambaye aliisaidia Chelsea kunyakua taji la EPL akifunga mawili dhidi ya Man City na Liverpool.

Zlatan Ibrahimovic wa Man United naye akipachika mawili dhidi ya Man City, Liverpool na Alexis Sanchez wa Arsenal yeye alifunga bao moja dhidi ya Chelsea.

Je, nani anayebisha kuwa United imeliwa kumsajili Lukaku ikiwa  washambuliaji wakali zaidi yake hawajamfikia kwa kutupia dhidi ya miamba sita EPL?

LihatTutupKomentar