Yanga mtumieni huyu kuziba pengo la Niyonzima



Kiungo wa klabu ya Zanaco na raiya wa Zimbabwe ameweka wazi nia yake ya kusakata kandanda katika klabu ya Yanga ambao ni mabingwa wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara.

Mshambuliaji huyo anaefahamika kwa jina maarufu la "RASTA" Zimiseleni Moyo ameweka bayana hili hivi karibuni wakati sekeseke la usajili likiendelea kulindima kila kona huku ligi nyingi zikiwa mapumzikoni.


Zimiseleni Moyo endapo atajiunga na Yanga basi huenda mashabiki  wakafuta machozi yaliyowatoka alipo ondoka kiungo wao Haruna Niyonzima.
LihatTutupKomentar