Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin De Bruyne , 28 amesema kwamba huenda akaondoka Manchester City iwapo marufuku yao itaidhinishwa.(HLN, via Manchester Evening News)
Roma inataka kumsaini mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa anaichezea Inter Milan, kwa mkopo kutoka Manchester United. (Sky Sport Italia, via Goal - in Italian)
Roma pia inataka kumuweka mchezaji aliyepo katika mkopo kutoka Manchester ambaye pia ni beki wa England Chris Smalling, 30, kwa msimu mwengine kulingana na mkufunzi Paulo Fonseca. (ESPN)
Winga wa Bayern Munich na Brazil Philippe Coutinho, 27, huenda akanyatiwa na Newcastle iwapo watamuajiri Mauricio Pochettino kuwa mkufunzi mpya wa klabu hiyo. (Mirror)
Lille wamepokea ofa ya Yuro 85m (£75m) kutoka kwa klabu isiojulikana kwa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anahitajika na Liverpool. (Telefoot - in French)
Real Madrid inapanga kuwauza takriban wachezaji watano msimu huu akiwemo winga wa Wales Gareth Bale, 30. (AS - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Leicester na Nigeria Wilfred Ndidi, 23, analengwa na klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain. (ESPN)
Newcastle na West Ham ni miongoni mwa klabu za ligi ya Premia kuweza kuulizia kuhusu mshambuliaji wa Real Madrid na Serbia Luka Jovic, 22. (90min)
Leicester huenda ikawasilisha ombi la kumnunua beki wa kushoto wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 22, iwapo beki wa kushoto wa England Ben Chilwell, 23, atauzwa. (Express)
Barcelona huenda ikamuuza mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez msimu huu huku klabu kadhaa za MLS nchini Marekani zikidaiwa kumuandama mchezaji huyo wa miaka 33. (Marca)
Newcastle, Everton, West Ham na Leicester zote zinachunguza hali ya kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 27. (90min)
Southampton ina matumaini ya kumsaini beki wa Reims na Ufaransa Axel Disasi, 22. (Mail)