Ally Ally wa Yanga afunguka haya

"Dirisha lilikuwa linafungwa usiku halafu siku hiyo hiyo nikaambiwa naenda kwa mkopo JKT Tanzania. . nilikataa nikawaambia nitabaki hapa hapa ntapambana kuhakikisha napigania namba kwa kuwa nna uwezo. . katibu akanijibu SAWA. . Baada ya hapo nikaona taarifa nimetolewa kwa mkopo. . nikawasiliana na katibu akanijibu ni lazima niondoke kwa mkopo. . nikampa masharti nitolewe kwa mkopo kwend KMC lakini Yanga SC wakakataa. . nilimuuliza katibu sijui hatma yangu kwa kuwa wenzangu walikuwa Singida na mimi nipo njia panda kiukweli sitoweza kuwasiliana naye tena kutokana na majibu aliyonipa ila akanisisitiza siwezi kujiunga na Yanga tena. . kama Yanga hawanitaki ni vema wakavunja mkataba wangu niwe huru kwa maana sasa sielewi hatma"

 -Beki wa Yanga SC, Ally Ally.
LihatTutupKomentar