MCHEZAJI HUYU SIMBA AFUNGUKA MENGI KUHUSU SIMBA SC



Beki wa klabu ya Simba, Kennedy Wilson ameibuka na kusema changamoto kubwa anayokutana nayo ndani ya kikosi cha timu hiyo ni mawasiliano baina yake na Wabrazil Tairone Santos da Silva pamoja na Wilker da Silva. 

Beki huyo aliyesajiliwa kutoka Singida United, ameeleza imekuwa shida kuelewana na wachezaji hao wakiwa nje ya uwanja kwani hawajui lugha ya Kiswahili wala Kiingereza. 

Kennedy amefunguka kuwa kutojua kwao lugha hizo mbili na yeye kutokifahamu Kibrazil inakuwa ni ngumu kwake kukaa kisha kupiga nao stori za hapa na pale sababu hawawezi kuelewana. 

Mbali na kutoelewana wakiwa nje ya uwanja, Wilson ameeleza pindi wanapokuwa ndani ya uwanja wanaelewana vizuri sababu lugha ya mpira inaeleweka. 

"Changamoto kubwa imekuwa ni kuelewana na Tairone pamoja na Santos sababu hawajui Kiswahili wala Kiingereza. 

"Inakuwa ngumu kukaa pamoja halafu tupige stori tunapokuwa nje ya uwanja sababu mimi pia sijui Kibrazil, mbali na hapo tukiwa uwanjani tunaelewana vizuri sababu lugha ya mpira inaeleweka. 

"Fraga yeye anaelewa Kiingereza hivyo inakuwa rahisi kwangu kuzungumza naye." 

Tangu atue Simba akitokea Singida United, Wilson amecheza mechi moja pekee ya Ligi Kuu ambayo ilikuwa dhidi ya Biashara United waliyoshinda mabao 2-0 huko Musoma, Mara
LihatTutupKomentar