YANGA WAFUNGUKA HAYA KUHUSU USAJIRI


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wake Mshindo Msolla, umetoa siku nne kwa wale wote wanaotumia nembo ya klabu kujinufaisha.  

Akiongea mchana wa leo Juni 28, 2019 makao makuu ya klabu Msolla amesema kwa wote wanaotengeneza jezi na vifaa vingine vya michezo waache mara moja. 

Msolla amesema kuwa itakapofika tarehe 30 mwezi huu, mtu yeyote atakayejihusisha na uuzaji wa jezi feki hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 

''Tunatoa siku nne, wote wawe wamejisalimisha na lengo la kuwaita watu hao wanaojihusisha na uuzaji wa jezi ni kufanya nao mazungumzo kujua ni namna gani wanaweza kusaidiana kwenye swala hilo la mauzo ya jezi na vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu''. 

Aidha ameongeza kuwa, "Tarehe 27/07 tutakuwa na matukio matatu, moja ni kutambulisha jezi, pili kutambulisha wachezaji wapya na tatu ni tutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki'', amesema. 

Pia amesesema Usajili wao umezingatia matakwa ya kocha mkuu Mwinyi Zahera. ''Tumesajili kulingana na matakwa ya mwalimu, hata huko alipo lazima atakuwa anafuraha maana wachezaji wote wa nje na ndani aliokuwa akiwahitaji tumewapata pia siku tatu zilizopita mwalimu alituma program ya mazoezi ,sisi kama menejimenti tumejipanga kuhakikisha yote yanaenda sawa

LihatTutupKomentar