UONGOZI wa Singida United umetangaza fursa kwa wachezaji wote ambao wanahitaji kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2019/20.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Catemana amesema kuwa lengo la mradi huo ni kutoa fursa kwa wachezaji wote wenye uwezo kuonesha ujuzi wao mbele ya benchi la ufundi.
"Hii ni fursa maalumu kwa wachezaji wote ambao wana uwezo kuonyesha ujuzi wao mbele ya benchi la ufundi lililo chini ya kocha, Felix Minziro na itafanyika kwa muda wa siku tano.
"Tutaanza jumatano ya Juni 12 uwanja wa Namfua, Singida ndani ya siku tano, gharama zote za malazi na chakula itakuwa ni juu ya mchezaji mwenyewe kwa muda wote wa majaribio," amesema Catemana.