KOCHA Mkuu wa KMC, Ettiene Ndayiragije amebeba tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Mei.
Ndayiragije ameongoza kikosi chake cha KMC kumaliza ligi kikiwa ndani ya nne bora baada ya kucheza michezo 38 licha ya kupanda ligi msimu wa mwaka 2018/19.
Kocha huyo amewashinda makocha wawili ambao ni Patrick Aussems wa Simba na Malale Hamsini kocha wa Alliance FC.