TP Mazembe inakutana na Simba kwa mara ya pili baada ya kupita kwa miaka minane
I
TP Mazembe yapata pigo Mputu augua Malaria, Malango majeruhi
TUESDAY APRIL 2 2019
Lubumbashi . TP Mazembe ina matumaini washambuliaji wake Tresor Mputu na Ben Malango watakuwa fiti tayari kuivaa Simba katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji mkongwe Mputu bado anaendelea na matibabu ya malaria wakati Malango ni majeruhi.
Mputu alicheza mechi ya mwishoni mwa wiki ambayo Mazembe waliyofungwa bao 1-0 na Saint Eloi Lupopo.
“Leo Jumanne, timu imefanya mazoezi mara mbili kabla ya safari ya kesho kuelekea Dar es Salaam. Katika mazoezi hayo Ben Malango alifanya pekee yake wakati Tresor Mputu akiendelea na matibabu yake ya Malaria aliyoanza tangu jana Jumatatu,” ilisema tovuti ya klabu hiyo.
Miamba hiyo ya DR Congo inavaa Simba, ambayo imezifunga Al Ahly na AS Vita katika mashindano ya msimu huu.
Uwanja wa Taifa ‘kwa Mkapa’, Simba inategemewa kuonyesha ushindani mkubwa kwa Mazembe, ambayo inasaka taji lake la sita la Ligi ya Mabingwa.