TFF YAWAPIGA RUNGU AZAM FC



Wachezaji watatu wa timu ya Azam FC wamekutana na rungu la Bodi ya Ligi  kwa kusimamishwa michezo mitatu na faini kiasi cha shilingi 500,000. 

Faini hiyo imekuja kutokana na kosa la kumzonga Mwamuzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Coastal Union dhidi ya Azam FC huko Tanga 

Wachezaji waliokumbwa na rungu hilo ni Ramadhani Singano, Tafazwa Kutinyu na Stephan Kingue Mpondo. 

LihatTutupKomentar