SIMULIZI:MBONA HAJIONGEZI? SEHEMU YA 01 Na GASPER WA MASTORY

MBONA HAJIONGEZI? SEHEMU YA 01
Na GASPER WA MASTORY
♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡
Wanafunzi wa chuo cha RUCO walizidi kutia umakini wao wote ndani ya darasa moja kwakuwa lecture(mhadhiri) aliekuwa akiwawafundisha alifundisha kwa haraka sana tena alikuwa hapendi kurudiarudia pale akisha fundisha kitu. kwakweli siku hiyo idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa lile hawakuambulia chochote.sijui zimwi gani lilikuwa limelikumba darasa lile baada ya dakika kuyoyoma.hatimaye kipindi kiliisha na wanachuo hao walipaswa kuwapisha wengine ili nao wapate wasaa wa kusoma. "brandon....brandon.."sauti flani ya kike iliita wakati watu wakizidi kutoka nje "ooh niambie vanessa"aliitika brandon baada ya kugeuka."daah mwenzio leo yani nimeambulia kujua tu kichwa cha somo vingine vyote patupu!..vipi wewe umempata yule lecture?"aliuliza vanessa. "ah mimi mwenyewe sio sana kidogo. tu"brandon akajibu "daah afadhali aisee..si utanielekeza na mimi eti?" "sasa hapo nashndwa kuahidi coz kidogo nna mambo mengi mengi so nahofia kuwa muongo" "camooooon brandon please nisaidie na mimi nipate hata concept yani?" vanessa akabembeleza "pouwa..tutacheki nikipata. tu mda tutafanya hivo usijali" "ntafurahi sana kwa kweli" "usijal mimi huwa napenda kila jirani yangu awe na furaha" "ahsante kwa ukarimu brandon" "your welcome"alimaliza brandon kisha wakaondoka huku wakipiga stori za hapa na pale.

****************************** *******************

"Haiwezekani Angel, atakuwa anakupenda sema tu wanaume wanatofautiana wengine kusema hawawezi wanakuwa na uoga flani hivi" aliongea binti mmoja katika chumba kimoja cha hosteli za chuo kile.
"ni kweli warda,hata mimi mwanzo nilifikiria hivyo lakini kadiri nnavomwona naona simwelewi yani daah nachanganyikiwa kwa kweli" alijibu angel kwa huzuni na kujiinamia chini "sasa ambacho hauelewi ni nini hapo?" aliuliza warda. "aah. yani ananijali kwa kweli,mcheshi na hata utanashati anao ila kila nikiwa nae ananiambia. tu stori nyingiiinee tu mfano majuzi  nilikuwa na stress balaa  baada ya kufeeli ile assignment ya Yule lecture ambaye haelewekagi kila afundishapo basi si nlikuwa nmekaa pale nje kwenye yale mabenchi nkiwaza sijui itakuwaje na yule lecture kanambia niirudie tena na ole nipate chini ya 8 sasa unajua ikawaje" akadokeza kidogo angel. warda na wenzie wawili wakaropoka "enheeee ikawaje" "basi bhana mola mwema nikiwa bado nawaza nikashangaa kumuona brandon anaketi jirani yangu.alinisalimia pale kisha akaniambia eti kama nina mda twende sehemu,ah kwakweli kwa mda huo nlikuwa nmevurugika yani skutaka kwenda popote nliona furaha yangu tu ni kukaa na  kutulia palepale.ila sasa Alinibembeleza pale nikaona isiwe shida nkamkubalia.basi tukaondoka skujua hata ananipeleka wapi. tulitoka nje ya chuo tukapanda bajaji tukaaanza safari mpaka kwenye barabara flani inayoenda kwenye lile jiweee kubwaaaa ambalo ukikaa hapo nje unaliona..basi shosti zangu si. tukapanda mpaka juu ya jiwe lile..daah unajua sijawahi kwenda kule jamani kumbe ni kuzuuuuri yani juu ya lile jiwe ni tambalare halafu pana ukubwa ambao ni sawa na uwanja wa netboli..kuna upepo mzuri,
siku hiyo kwakua ilikuwa jioni ndo inaanza hata hakukuwa na jua kali." akameza mate kidogo
" mara brandon akatoa juisy mbili za mirija kwenye begi lake alilokuwa amelibeba. na biskuti moja kubwaa akaifungua na kunipatia kipande kama ananilisha hivi akanipatia na juisy.kwakweli nilihisi furaha sana ingawa nilikuwa na huzuni sana siku hiyo ila nilijihisi furaha sana nikiwa pale juu ya lile jiwe. huzuni wote niliufyekelea mbali" angel alisema huku akitabasamu kidogo. halafu akaendelea "sasa jambo la kushangaza nkamuona brandon anatoa...........ITAENDELEA......angel atatoka salama kweli? usikose..like page yangu ya simulizi tamu za gasper kwa mastory zaidi...whatsapp 0656322828.

LihatTutupKomentar