Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy leo asubuhi ameomba mwongozo kwa Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson akiwataka wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania kuichangia klabu ya Yanga.
Keissy ametoa ombil hilo akisema anataka waichangie Yanga kwa kukatwa fedha 50,000 hadi 100,000 kwenye posho zao za leo ili kuisaidia klabu ya Yanga ila hoja hiyo ilipigwa chini na wabunge wengi.
Baada ya hoja yake kukataliwa na wabunge wengi, Keissy ameitaka serikali waiingize klabu ya Yanga kwenye mpango wa mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF).
Amefuguka kwa kuitaka serikali iingize Yanga kwenye mfuko huo unaofanya kazi kusaidia kaya maskini ili wapatiwe msaada ambao utawasaidia kujinasua kwenye ukata wa fedha unaoikabili klabu hiyo