YANGA YATINGA ROBO FINAL ASFC

Yanga SC imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) kwa kuichapa Namungo FC bao 1-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi. Goli pekee la Yanga limefungwa na Heritier Makambo dakika ya 83 akimalizia kwa kichwa krosi ya Deus Kaseke licha ya Namungo kuonesha soka la upinzani wa hali ya juu huku wakipoteza nafasi zaidi ya mbili za wazi walizotengeza. Hili hapa goli la Makambo

LihatTutupKomentar