MWINYI ZAHERA ATOA TAMKO HILI TFF


Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Singida United ya mjini Singida, Kocha Mwinyi Zahera amefunguka tena kuhusiana na ratiba ya ligi.

Zahera ameeleza hakika ratiba imekuwa si rafiki kwao ukiangalia kumekuwa na changamoto ya usafiri kutumia umbali mrefu wakiwa kwenye gari.

Zahera amesema wanapatwa na uchovu kwani tena wanapaswa kurejea Tanga kwa ajili ya mechi dhidi ya JKT Tanzania.

Amewataka Bodi ya Ligi kupitia TFF kuwa wanapaswa kujipanga kwakuwa wachezaji wake wanachoka na wanaweza wasihimili mikimikiki ya ligi kwasababu wanakuwa wanatumia nguvu nyingi.

Katika mchezo huo wa jana, Yanga ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na ukiwa na mchezo wake wa pili ikikosa alama mbili baada ya Coastal Union ambayo walienda nayo sare ya 1-1.

LihatTutupKomentar