JINSI KIBURI CHA WAARABU KILIVYOIGHARIMU SIMBA

Na Emmanuel Mkome
Mohamed Aboutrika endapo kama angeenda Ulaya mapema huenda leo hii angekuwa na jina kubwa kama la Mohamed Salah. Lakini aliponzwa na jambo moja tu. Kiburi.Hivi karibuni winga Ramadan Sobhi katoka Hundersfield ya ligi kuu England karudi kwao Al Ahaly kwa mkopo. Sidhani kama atarudi tena.Waarabu wana kiburi. Lakini hapo hapo tujiulize kwanini waarabu wa Misri wana ujasiri huo? Jibu ni moja tu kwamba ligi yao ni bora. Ligi yao ina ushindani wa kati.
Hivyo basi huwa wanatazama mishahara ya timu za Ulaya na badae wanalinganisha na ya kwao wanaona tofauti ni ndogo sana hivyo wanaamua kubaki Misri. Wengi wao huwa wanaenda Ulaya kuzuga tu wakiwa umri tayari umesogea. Kaka yangu Amri Zaki ni mmoja wapo. Ndio maana hata katika kikosi chao cha timu ya Taifa Misri wana mchezaji mmoja tu mwenye kiwango cha dunia ambaye yeye inavyoonekana kakishinda kiburi hiki. Ni Mohamed Salah tu.
Ni uhalisia ambao nchi kama Tanzania huwa hatutaki kuukuubali. Yaani kuna mashabiki wa Simba au Yanga huwa wanaamini kabisa kuwa timu zao zinaweza kwenda kucheza na Raja Casablanca au TP Mazembe ugenini na zikashinda mabao hata 4-0. Ni uwongo Ni muda wa kukaa chini na kuangalia wapi tumekosea. Lengo ni kuifanya ligi yetu iwe bora kwa kuharibu mfumo mzima wa soka uliopo sasa hivi na kuleta mfumo mwingine mpya. Vinginevyo hizi tano tano zitaendelea kutuhusu
Waarabu wengi wa Misri huwa wana kiburi. Sina maana ya hali ya kutokuwa na nidhamu. Hapana. Namaanisha kuwa wachezaji wengi wa kiarabu kutoka Afrika ya kaskazini hasa Misri huwa wanathamini sana na kukumbatia vitu vyao. Mara nyingi huwa hawana papara ya kwenda kucheza soka barani Ulaya. Wengi wao huwa wanamalizia soka lao katika miji ya Cairo au Alexandria. Hichi ndicho kiburi cha waarabu wa Misri.Mohamed Aboutrika ni miongoni wa wachezaji wa namna hiyo.
Ni uhalisia ambao nchi kama Tanzania huwa hatutaki kuukuubali. Yaani kuna mashabiki wa Simba au Yanga huwa wanaamini kabisa kuwa timu zao zinaweza kwenda kucheza na Raja Casablanca au TP Mazembe ugenini na zikashinda mabao hata 4-0. Ni uwongo Ni muda wa kukaa chini na kuangalia wapi tumekosea. Lengo ni kuifanya ligi yetu iwe bora kwa kuharibu mfumo mzima wa soka uliopo sasa hivi na kuleta mfumo mwingine mpya. Vinginevyo hizi tano tano zitaendelea kutuhusu
LihatTutupKomentar