RUFIJI UNITED WATANGAZA KIAMA KWA MTIBWA SUGAR

Kikosi cha Kiluvya United ambacho kwa sasa kimebadili jina na kuitwa Rufiji United kimewatangazia vita kali Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo  wa kombe la Shirikisho utakaopigwa leo uwanja  Manungu, Morogoro.

Rufiji United ambayo kwa sasa ipo chini ya Mohammed Mchengerwa imejipanga kuitungua mabao 3 na kuwatoa kwenye reli mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Ofisa habari wa Rufiji United, Stephen Kinabo amesema kikosi kimejipanga kiasi cha kutosha kuleta changamoto mpya kwa wapinzani.

"Tunatambua ubora wa Mtibwa Sugar na hasira walizonazo baada ya kutoka kwenye mashindano ya kimataifa, ila tumejipanga  kuwashushia mvua ya mabao kama 3 hivi," alisema

LihatTutupKomentar