RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA (TPL)

Ratiba Ligi kuu ya Tanzania bara TPL leo 9 December 2018

Ligi kuu soka ya Tanzania bara itaendelea leo 9 December 2018 katika nyasi za Viwanja tofauti

Jumla ya Mechi mbili zitachezwa leo ambapo mechi ya Kwanza itazikutanish Coastal Union ambao watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.
)
Na Mechi ya Pili itaanza majira ya saa moja Usiku ikizikutanisha Yanga ambao watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mkoani Mara.

Yanga imethibitisha kuwakosa nyota wake Ibrahim Ajibu mwenye kadi 3 za Njano na Mrisho Ngassa ambaye anatumikia adhabu ya Kukosa mechi 3 baada ya kupewa kadi nyekundu.

hata hivyo kuna wachezaji watatu watarejea katika kikosi cha Yanga ambao ni Papy Tshishimbi, Gadiel Michael na Kelvin Yondani ambao walikuwa majeruhi

LihatTutupKomentar