MZEE AKILIMALI AFUNGUKA HAYA MEENGI KUHUSU YANGA

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, ametoa baraka zake zote kuelekea uchaguzi mkuu wa Yanga utakaofanyika Januari 13 2019.

Akilimali ambaye alikuwa sambamba na Baraza la Wazee wa Yanga, amesema wapo wapo tayari kuelekea uchaguzi huo ambao utakuwa ni wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi ili kuwapata mbadala wao.

Aidha, Akilimali amepingana na suala la mkutano mkuu wa dharura Yanga kufanyika akiamini italeta uchonganishi kwa Baraza la Michezo nchini (BM), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali kwa ujumla.

Kutokana na kuukataa mkutano huo, Akilimali ameshauri ni vema zaidi Yanga ikazidi kuweka nguvu zake kuelekea uchaguzi mkuu pekee ambao utakuwa na manufaa kwa klabu.

"Kufanya mkutano mkuu ni uchochezi kwa serikali, BMT, TFF maana italeta uvunjifu wa amani na uchochezi kwa serikali yetu. 

Hatuna budu kutoa onyo kwa wajumbe wetu watatu waliobaki kuwa kuendelea kukaidi maagizo ya serikali, ni kuonesha utovu wa nidhamu mbele yake" alisema.

LihatTutupKomentar