MO" SALAH, SADIO MANE VITA KALI TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRICA

MSHAMBULIAJI wa Misri, Mohamed 'Mo' Salah atatetea tuzo yake Mwanasoka Bora wa Afrika dhidi ya mchezaji mwenzake wa  wa Liverpool, Msenegal Sadio Mane.
Mane na Salah ni kati ya wachezaji 10 walioingia fainali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika inayotolewa na Shirikisho la Soka Afrika. 
Wengine ni Alex Iwobi wa Nigeria na Arsenal, Andre Onana wa Cameroon na Ajax, Mehdi Benatia wa Morocco na Juventus, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Arsenal na Riyad Mahrez wa Algeria na Manchester City.


Orodha hiyo inakamilishwa na wachezaji watatu wanaocheza klabu za Afrika, ambao ni Anis Badri wa Tunisia na Esperance ya kwao, Denis Onyango wa Uganda na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Walid Soliman wa Misri na Ahly ya kwao.
Mshindi atapatokana baada ya kura zitakazopigwa Maofisa wa Idara ya Habari ya CAF, Magwiji, Makocha wa timu zilizofika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika na makocha na Manahodha wa timu za taifa 54 wanachama wa CAF.
Tuzo itatolewa katika hafla maalum itakayofanyika Jumanne ya Januari 8 mwaka 2019 mjini Dakar, Senegal.
Mwaka huu, Salah alishinda tuzo hiyo akiwabwaga Mane na Aubameyang wakati akiwa Borussia Dortmund bado kabla ya kuhamia Arsenal msimu huu.

LihatTutupKomentar