HAWA HAPA WACHEZAJI SIMBA KUIKOSA NKANA FC

imba: Wachezaji watakaokosekana dhidi ya Nkana leo

Leo ndiyo leo ambapo mabingwa wa soka nchini Tanzania watashuka dimbani kucheza na Nkana Fc kutoka Zambia katika mechi itakayoamua hatma ya Timu mojawapo kufuzu hatua ya makundi barani Afrika.

Kuelekea mchezo huo Simba itakosa nyota wake mmoja ambaye inaelezwa kuwa anakosa mchezo huo kutokana na Kupata majeraha wakati huu Simba Ikijiandaa na mchezo huo wa Nkana Fc.

Mchezaji ambaye atakosekana ni Mohammed Ibrahim (Mo Ibrahim) ambaye hata hivyo amekuwa hana nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha Kwanza cha Mbelgiji Patrick Aussems.

Simba msomaji wa MKOMESPORTNEWS simba itahitaji kupata ushindi walau wa bao 1 tu kwa 0 ili kuweza Kufuzu hatua inayofuata , Hatua ya Makundi ambayo Tanzania haijafanya hivyo kwa timu zake kwa takribani miaka 15 sasa

LihatTutupKomentar