Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga kwenye klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji amewapa somo zito viongozi wa Yanga kutokana na juhudi zake pamoja na uendeshaji wa klabu yake ilivyo katika uendeshaji.
Ofisa habari wa Yanga, Dismass Ten amesema kuwa kwa hatua ambayo amefikia Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Starz' yapaswa kuwa funzo kwa wengine kuweza kufuata nyayo zake.
Samatta amepewa heshima kwa kuchapishiwa jezi maalumu yenye nembo ya Golden Bull kufuatia kufanikiwa kutupia mabao 10 kambani na kumfanya kuwa kinara katika orodha ya wafungaji kwa sasa.
"Umestahili heshima kwa juhudi ulizoonesha kwa kufunga mabao 10 hadi sasa kapten, nimejifunza namna ambavyo klabu zinaendeshwa zina uwezo wa kumiliki mashine za uchapishaji wa aina zote na linapokuja suala la kuprit jezi iwe namba au majina mambo yanakamilika hapo hapo na sio kwa mdosi," alisema.
Nyota huyo alisajiliwa na klabu hiyo akitokea TP Mazembe ambayo pia ilimnyakua kutoka Simba SC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.