YANGA WAAPA KUWAPIGISHA KWATA JKT TANZANIA


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Mrisho Ngasa amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kushuhudia namna watakavyoonyesha uwezo mbele ya JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu.

Ngasa amekuwa katika ubora wake baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi katika moja ya mchezo waliocheza kanda ya ziwa dhidi ya Mwadui FC baada ya kufunga bao safi nje ya 18.

"Mashabiki watupe sapoti kwa kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa nasi tunahitaji kufanya vizuri ili tuweze kupata pointi tatu, kwa mbinu ambazo tumepewa tuna imani tutafanya vizuri," alisema.

Yanga wamecheza michezo 12 bila kupoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa wakiwa na pointi 32 wakiachwa kwa pointi moja na vinara Azam FC wenye pointi 33.

LihatTutupKomentar