TFF YAMFUNGIA MWENYEKITI WA KAMATI YAKE

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Maadili limemfungia maisha kutojihusisha na soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati yake ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kimaadili. 

Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya TFF, Wakili Hamidu Mbwezeleni alisema Kuuli akitambua nafasi yake ndani ya shirikisho hilo, alifanya makosa hayo matatu ambayo kimsingi yanastahili adhabu ya kifungo cha maisha kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu. 

Makosa matatu ambayo yamemtia hatiani Wakili Kuuli ni kusambaza nyaraka za shirikisho kinyume na kanuni na taratibu, kutoa maelezo yanayoonesha kuwa na mgongano wa kimaslahi kwa kuwapa watu wasiohusika na pia kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya shirikisho. 

"Uamuzi huu umechukuliwa kwa kufuata kanuni na taratibu. Hakuna aliyemuonea Kuuli niliweke hilo sawa," alisema Wakili Mbwezeleni.

LihatTutupKomentar