FABREGAS, FABINHO, SUAREZ: TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO IJUMAA



Chelsea huenda ikabadili msimamo kuhusu mpango wake wa kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 27,kutokana na kuimarika kwa mchezo wa Ross Barkley, 24, na Ruben Loftus-Cheek, 22. (Star)

Huku hayo yakijiri, Liverpool imefutilia mbali uwezekano wa kiungo huyo wa kimaatifa wa Wales ambaye yuko tayari kuondoka Gunners bila malipo msimu wa joto kujiunga nayo. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Mhispania Cesc Fabregas, 31, atalazimika kusubiri hadi mwaka mpya kabla ya kuanza mazungumzo ya kandarasi mpya na Cheasea . (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 31, anasema Barcelona hivi karibuni itaanza kumtafuta mtu atakaechukua nafasi yake licha ya kufunga hat-trick katika mechi ya El Clasico. (Sport 890, via Sun)


Liverpool inajiandaa kumpatia kandarasi mpya mlinzi wa England defender Joe Gomez, 21, miaka tatu na nusu hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Brazil Fabinho huenda akaondoka Liverpool miezi sita tu baada ya kuhamia Anfield kwasababu ''ameboeka''. (Le Parisien - in French)

Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema "Hatutapoteza muda wetu kujadili hilo" alipoulizwa kuhusu tetesi za Real Madrid kutaka kumpatia kazi kama meneja wake mpya. (AS, via VTM Nieuws)

Tottenham inapania kumnunua kiungo wa kati wa Watford, mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25. (Mirror)

Meneja wa Manchester United boss Jose Mourinho ana mpango wa kufanya usajili zaidi ya moja wakatu dirisha la uhamisho litakapo funguliwa mwezi Januari- Ni mara ya kwanza klabu hiyo itafanya hivyo katika kipindi cha miaka 10. (Manchester Evening News).



LihatTutupKomentar