SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA. MTUNZI;RAJA SAIDY. WHATSAPP;0756920739.

SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.

SEHEMU YA KWANZA 
  
"Dada amka tusali amka dada"
"Nina usingizi mdogo wangu"
"lakin dada sio vizuri kulala bila kusali"
"mdogo wangu nimechoka kwani kutokusali siku moja tutahathirika na nini,we tulale bwana"
"sawa dada ila sio vizuri"
"we lala bwana"
"Caro kwani mama na baba wamesha lala?"
"Ndio dada"
"sawa tulale"
"sawa"

........*****...............*******...............

  usiniuwe,usiniuwe mama usiniuwe...............lazima nikuuwe mwanangu napenda sana damu,hahahahahahahahah.

Nilishtuka kutoka kwenye ndoto hiyo ya maajabu huku jasho likiwa limenitanda mwili mzima,kutokana na uoga niliyokuwa nao juu ya ndoto hiyo na kuhaidi kuwa nitamueleza mama juu ya ndoto ile iliyokuwa ikimuhusu yeye.nilitazama pembeni yangu tayari mdogo wangu Caro aliyekuwa akinisihi tusali kabla ya kulala tayari alikuwa katika usingizi mzito huku akiendelea kutoa sauti mithili ya mtu anayechunga mifugo yake.
"Caro,caro,caro.."
"Abee dada"
"Amka mdogo wangu"
"kuna nini dada????"
"we amka"
mdogo wangu alimka kisha akaanza kupekecha macho yake ili apate kuona vizuri,kisha akanitupia swali?
"Dada kuna nini halafu ujui muda umeenda tunatakiwa kulala"
"Caro mdogo wangu nimeota ndoto mbaya kuhusu mama tena anataka kuniuwa"
"kukuuwa?"
"Ndio"
"mama yetu huyu??"
"si ndio mdogo wangu mbona una maswali mengi"
"dada nadya heli ungekuwa umeota ndoto kuhusu hata baba au hata mpenzi wako ningekusikiliza lakini kuhusu mama hiyo sio ndoto tena  maana vyote ulivyoviota ni vya uongo"
"Caro mdogo wangu niamini"

Mdogo wangu caro alivuta shuka bila ya kuniongelesha kitu chochote,nikiwa bado ni mwenye hofu kubwa na kushindwa kupata usingizi kabisa.huku
Nikiwa nimeuwegemea mto wangu vyema pia kidole changu cha mwisho katika mkono wa kulia kikiwa mdomoni. macho yangu yaliendelea kutazama juu ya paa la nyumba yetu kwa lengo la  kufikiria ndoto ile,hivi itawezekanaje mimi kumuotea mama yangu mzazi tena kwa mabaya haiwezekana lazima nifanye uchunguzi yes.
      Baada ya kuwa nimeshapata jibu nini cha kufanya nilivuta shuka kama kawaida ili niweze kupata usingizi.

..........********...........*********
Mwanangu nadya namuuwa baba yako,atakayefuata ni mdogo wako caro pia  wewe utakuwa wa mwisho,hahahahahaha.

      Nilishtuka kutoka katika ndoto ile iliyokuwa ya pili kwa siku moja,tena ndoto mbaya heli ya kwanza maana ndoto hiyo haiwezekani hata  kusahaulika katika siku zote.
      Nilivuta shuka la mdogo wangu caro kwa lengo kumuamsha.
"dada mbona unapenda kunionea hivyo????"
"sio nakuonea mdogo wangu amka kumekucha"
"amna bana niache nilale nadya"
"poa"

Nilishuka kutoka kitandani kwangu huku nikimuacha mdogo wangu caro aendelee kuuchapa usingizi,kichwani kwangu nilitawaliwa na wazo kuu moja tena kuhusu ndoto mbaya nilizoziota juu ya mama yangu.
"Au itakuwa mama ni mchawi nini,ila sio kweli kwa sababu yeye ni mtakatifu siku zote sikuwahi kumuona anajihusisha na uchawi itakueje nimuotee vibaya,hizo ni ndoto tu hazina madhara"
  Nilipiga hatua zangu za kuelekea mpaka mahali mlango ulipo,kisha nikaufungua.nilikaribishwa na mwanga hafifu wa jua.nilielekea mpaka kwenye chumba cha mama kisha nikagonga,
"Nani?"
"mama ni mimi mwanao nadya,shikamoo?"
"marahaba,asubuhi yote hii kuna nini,au unataka ukorofishane na baba yako??"
"halafu mama umenikumbusha hivi baba  amelala???"
"Ndio mwanangu"
"shikamoo baba??"
"mbona haongei???"
"hata mimi nashangaa namuona kajikunyata hata haongei"
"hebu mama fungua mlango"
   Baada ya muda mchache mama alifungua  mlango kisha akapiga hatua za kuelekea kitandani kwake,pia na  mimi nilifanya hivyo hivyo kama mama,nikiwa tayari niko ndani ya chumba cha mama ghafla nilimkuta baba kwenye kona ya chumba hicho,huku akiwa anatokwa na udenda mithili ya dondocha,jambo lililonifanya nipige kelele,
"caro,baba anakufa caro......"
"mama kamgeuza dodocha"

nilivyomaliza kuongea hivyo baba alipotea katika eneo lile huku mama akiendelea kunikazia macho wakati akiwa pale pale kitandani.
"mwanangu nadya baba yako kaisha fariki,mimi ndo nimemuuwa mwili wake huko hapa kitandani ule uliyokuwa unauona ulikua mzimu wake tu"
  je nini kitaendelea........
   kama unataka muendelezo Nitafute whatsapp namba 0756920739 au sms namba 0621047841.

LihatTutupKomentar