MWINYI ZAHERA AFUNGUKA KUHUSU HUYU MCHEZAJI KUTOKA GHANA


Usajili Dirisha Dogo: Yanga wahamia kwa Mghana Zahera afunguka

Taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa tayari Zahera ameleta kifaa kipya Jangwani.
Akizungumza na nasi jana, Zahera alisema kuna mchezaji ambaye alimuona nchini Ghana na kuridhishwa na uwezo wake mkubwa na tayari alishawaonyesha baadhi ya viongozi video zake ili wamalizane mapema.
Alisema huyo Mghana ni mzuri na endapo Mwenyekiti wa timu, Yusuph Manji, atarudi kama ambavyo amepenyezewa taarifa, itakuwa vizuri zaidi, kwani atafanya usajili wa nguvu.

“Msiwe Na mashaka, kwani kuna mchezaji kutoka Ghana nimemuona na nimeshawaonyesha baadhi ya viongozi video zake, ni moja ya mastraika wenye ubora wa hali ya juu.
“Nadhani tukimpata huyo hatutakuwa na shida sana, pia nimesikia Mwenyekiti wa timu (Yusuph Manji), muda wowote anarejea, itakuwa vizuri sana, kwani akimwaga fedha nitawaletea wachezaji wazuri kama ilivyo kwa TP Mazembe,” alisema.

LihatTutupKomentar