MSAFARA WA MENEJA WA YANGA WASIMAMISHWA N

Meneja wa Yanga Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye alikuwa nahodha wa zamani ndani ya kikosi hicho jana alifanyiwa 'sapraiz' ya aina yake kutoka kwa mashabiki wa Yanga wa kijiji cha Chigugu kilichopo Mtwara. 

Mashabiki hao walikuwa barabarani kusubiri msafara wa Cannavaro uliokuwa unaenda kufungua tawi la Yanga mkoani Mtwara. 

Msafara huo ukiwa njiani ulisimamishwa na mashabiki hao ambapo wazee wa eneo hilo walimkabidhi Cannavaro katoni nne za maji huku wakimwambia akirudi apitie kuchukua kuku wake kama zawadi. 

Yanga wamekuwa na matokeo mazuri msimu huu kwani katika michezo 8 waliyocheza wamefanikiwa kushinda saba na kutoa sare mchezo mmoja huku wakiwa na pointi 22 na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

LihatTutupKomentar