MBONA HAJIONGEZI?   SEHEMU YA 05 na GASPER WA MASTORY

MBONA HAJIONGEZI?
  SEHEMU YA 05
na GASPER WA MASTORY
♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡
ILIPOISHIA
baada ya kuwafikia walipo aliwatazama kwa jicho flani la wivu kisha SONGA NAYO akamsalimia Brandon
‘’mambo?’’
‘’powa niambie’’
‘’si unaenda hivi class?’’ ‘’yah naenda”
“twende basi, na mimi naenda huko’’
‘’poa poa’’ wakati huo angel alikuwa kimya tu akisikiliza tu mazungumzo yao.
‘’angel kachukue basi daftari zako utatukuta class sisi tunatangulia’’alisema Brandon,angel hakujibu kitu aliitikia tu kwa kichwa tu na kuondoka taratibu kinyonge sana alionekana dhahiri hakupenda kumwacha brandon aondoke na vanessa.

Darasani masomo yaliendelea. siku zikazidi songa huku ukaribu ukizidi kujengeka kati ya Brandon na Vanessa na kwake angel kwa Brandon kila mmoja alikuwa jirani na Brandon kwa wakati wake mara vannessa wawe na Brandon uwanjani,siku nyingine angel alionekana na Brandon katika garden wakisoma pamoja. Hali ya wivu ikaanza kumjaa kila mmoja wao kila alipomwona Brandon akiwa na mwenzake.Ilihali mpaka wakati huo Brandon hakuwa amempajibu lolote angel juu ya ombi lake hata upande wake Vanessa yeye hakuwa amemwambia chochote kijana huyo zaidi ya kupenda kuwa karibu na Brandon ilimradi tu moyo wake usuuzike Vanessa hakuweza umwambia chochote Brandon ila alimpenda Brandon hakuna mfano yani kila alichokifanya Brandon kwake alikiona kizuri alijitahidi kujionesha mkamilifu mbele ya Brandon,Brandon naye hakuacha kuwaheshimu wote kama marafiki zake ingawa alitambua angel anampenda sana ila hakujua chochote kuhusu Vanessa kwakuwa yeye hakuwa muongeaji kama ilivyokuwa kwa angel.

Mchana mmoja tulivu Vanessa alimwomba Brandon waende sehemu wakatembee,Brandon aliitazama ratiba yake akaona hakuwa na jambo lolote mbele yake,bila hiyana akamkubalia binti Yule aliyeonekana kwao hela haikuwa tatizo ila tatizo lilikuwa namna ya kuitumia hiyo hela. ‘’tutarudi kama saa ngapi hivi?’’aliuliza Brandon ‘’saa 12 jioni hivi,si sawa afu mbona leo hatuna vipindi tena mpaka kesho bhana’’ ‘’sawa.nilikuwa naangalia kama nitawahi kurudi nataka nikajisomee’’
‘’we twende hatutachelewa nakuahidi ondoa wasiwasi tafadhali’’ alisema Vanessa huku akimshka mkono Brandon kama ishara ya kubembeleza
‘’haya bhana mimi sina neno twende.’’

Vanessa alitabasamu akamshika mkono brandon,kisha walichukua tax na kuondoka katika upeo wa  chuo kile

****************************** ****************************** * Baada ya kufaulu vyema katika masomo yake katika kiwango cha GPA ya point 5,Marina alikuwa na sifa za kuwa mkufunzi wa chuo chochote hapa Tanzania,ule usemi wa wahenga eti ‘kizuri chajiuza kibaya chajitembeza kweli’ ulithibitika dhahiri, vyuo kibao vilishindana dau ili kumpata mwanadada huyo aliekuwa na miaka 24 tu vyote vikimuhitaji awe lecture wa chuo chao. Jambo ambalo lilimfanya marina ajivunie elimu aliyonayo,sasa kilichokuwa kimebaki ni yeye tu uchagua ni wapi aende. Jibu lake lilitia tiki katika chuo cha RUCO ambacho kwanza kilikuwa kikimilikiwa na taasisi binafsi hivyo dau lake lilikuwa nono kweli pia chuo hicho ilikuwa katika miongoni mwa mikoa ambayo marina aliihusudu vilivyo,iliuwa ni tofauti sana kwake kwani licha ya kukulia jijini dar es salaam,hakulipenda jiji hilo tena na joto lake ndo kabisaa hivyo aliona ni bora akafanye kazi mbali na jiji hilo. Na ndipo akaamua kukubali ombi la chuo hicho cha RUCO cha mkoani Iringa,hakujali baridi linalosifika mkoani humo lakini alitamani kuona anaishi sehemu ambapo yeye roho yake itaridhia. Baada ya taratibu zote kukamilika,marina alianza kazi rasmi katika chuo hicho akiwa kama mkufunzi mpya.kutokana na utaratibu wa chuoni hawakusanyiki kama shle ya msingi hivyo hakuna aliyetambua kuwa marina mi lecture wengine walidhani ni mwanachuo mgeni kutokana na hakuna aliyekuwa ametambulishwa kuwa yeye ni nani,labda wanafunzi wa darasa lake ndio walitegemewa kumfahamu lecture huyo mgeni.

****************************** * Kelele zilikuwa zikiendelea katika chumba kimoja cha kusomea chuoni hapo huku watu wakijibizana huku na kule,ilionekana dhahiri kuna jambo halikuwa sawa. ‘’hapana bhana nyie mnaona kama mimi sifanyi kazi eeh,najitahidi kuzipeleka assignment zenu kwa lecture kwa wakati kadri ya nyie mnavyo ziwasilisha kwangu ila mimi sijui tatizo liko wapi mnaona kama mimi ndo sababu ya nyie kupata marks mbovu,sasa niwaambie tu fanyeni mnachofanya ila msinitishetishe bhana mi mwenyewe nna mambo kibao ya kufanya’’ aliuwa kiongozi wa darasa au kama wanavyomuita CR akijaribu kujitetea baada ya wanadarasa lake kuchoshwa na tabia yake ya uvivu na uzembe wa kuchelewesha kufikisha kazi zao kwa wakufunzi jambo lilipelekea wanafunzi wengi wapunjwe marks zao. ‘’atoke si hatumtaki bwana’’ ‘’tumpindue achaguliwe mwingine kwani yeye nani hata tumnyenyekee’’ ‘’kweli bwana achaguliwe mwingine au nyie mnaonaje?’’ ‘’ndiooooooooooooooooooooo’’ zilisikika sauti kadhaa za wanadarasa na hatimaye wakakubaliana wachague kiongozi wa darasa mwingine kumbadili Yule asiyewajibika
‘’jamani mimi naona warda anaweza kuwa CR mzuri’’ mmoja alipendekeza ‘’weeeeeeee ishia hapo hapo mimi sijawahi kuwa hata hata kiongozi wa chekechea sembuse vichwa vyote hivi ntaviwezea wapi,akaaaa! mi siwezi jamani’’ warda alidakia haraka baada ya kupendekezwa bila ya yeye mwenyewe kuridhia ‘’jamani mnaonaje Brandon awe CR’’mwingine aliropoka...........ITAENDELEA.......Haya sasa mambo huku darasani yamewaka...na huyu marinna ndo itakuwaje duh...yajayo yanafurahisha....uskose...Nenda kalipe page yangu inaitwa simulizi tamu za gasper kwa story nyingine kali.

LihatTutupKomentar